Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 29, 2024 Local time: 21:44

Marekani yasonga mbele kuimarisha usalama wa bandari dhidi ya udukuzi


Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Marekani Joe Biden

Rais Joe Biden Jumatano anatarajia kutoa amri ya kiutendaji itakayo wapa majukumu Walinzi wa Pwani wa Marekani kusimamia usalama wa mitandao katika bandari na majengo mengine ya shughuli za baharini, ikiwa na lengo la kuhakikisha kuwa kuna usalama wa kiasi unaohitajika katika maeneo hayo haraka iwezekanavyo.

Amri hiyo pia itawaruhusu Walinzi wa Pwani kufanya ukaguzi wa usalama wa mitandao wa majengo yote na meli, na hata kudhibiti upitaji wa vyombo vya baharini vinavyo shukiwa kuwa ni tishio la udukuzi wa mitandao kwa bandari za Marekani.

Mabadiliko hayo pia yanataka lazima kuripoti shambulizi lolote la udukuzi wa mitandao katika majengo ya shughuli za baharini.

Bandari ya Los Angeles, on Oct. 20, 2021, huko San Pedro, Calif.
Bandari ya Los Angeles, on Oct. 20, 2021, huko San Pedro, Calif.

“Kuendelea kwa operesheni kwenye bandari za Marekani kuna athari za wazi na za moja kwa moja kwa mafanikio ya nchi yetu, uchumi wetu na usalama wa taifa letu,” naibu mshauri wa Usalama wa Taifa wa White House Anne Neuberger aliwaambia waandishi. “Shambulizi la mitandao linaweza kusababisha uharibifu mkubwa, kuliko dhoruba au tishio jingine la vitendo.

Kuna zaidi ya bandari 300 nchini Marekani, zinazo ajiri takriban Wamarekani milioni 31. Maafisa wa Marekani wanasema bandari hizo zinachangia takriban trilioni 5.4 kwa uchumi wa nchi na wakati huo huo zikihudumu kama vituo vikuu vya kuingia kwa mizigo kutoka duniani kote.

“Kitu chochote kitatakacho vuruga [Mfumo wa Usafiri wa majini] MTS, iwapo ni kitendo cha binadamu au tukio la asili, harakati au kimtandao, kina uwezo wa kusababisha athari mbaya kwa mfumo wa usambazaji wa bidhaa za ndani na za kimataifa,” alisema Mkuu wa Jeshi la Majini John Vann, kamanda wa Kamandi ya Ulinzi wa Mitandao ya Pwani.

Amri ya kiutendaji, alisema Vann, inawapatia Walinzi wa Pwani “ mamlaka ya wazi kuchukua hatua wanapokabiliwa na vitisho vya udukuzi wa mitandao.”

Tayari, maafisa wa Marekani wametoa onyo kuhusu kuwepo zaidi ya meli zilizotengenezwa China zenye zana za kupakua mizigo nchi kavu zaidi ya 200, zinazotumika kupakia na kupakua mizigo katika bandari na majengo kote Marekani.

“Jinsi zilivyotengenezwa, hizi kreni zinaweza kudhibiti, kufanyiwa ukarabati na kuandaliwa programu zake kutoka maeneo ya mbali,” Van alisema, akisema kuwa hivi vifaa “vinaweza kutumika kufanya hujuma.”

Awali, jarida la Wall Street liliripoti kuwa maafisa wa ulinzi wa Marekani wameelezea wasiwasi wao kuwa kreni hizi zingeweza kutumika na China kufanya ujasusi wa mali ghafi zinazo safirishwa kuingia na kutoka Marekani.

Ripoti ya Jeff Seldin wa VOA

Forum

XS
SM
MD
LG