Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 20:18

Marekani na nchi nyingine zinailaumu China kwa udukuzi wa mitandao


Picha yenye mfano wa udukuzi wa mitandao
Picha yenye mfano wa udukuzi wa mitandao

Marekani na nchi kote duniani, zinaiwajibisha Jamhuri ya watu wa China (PRC), kwa mtindo wake wa tabia isiyo ya uwajibikaji, usumbufu katika mtandao wa wavuti ambao unaleta tishio kubwa kwa usalama wetu wa kiuchumi na kitaifa, ilisema taatifa kutoka waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken

Marekani na nchi nyingine zinaishutumu wizara ya usalama ya serikali ya China kwa kutumia wadukuzi wa mikataba ya jinai kufanya operesheni zisizoidhinishwa za mtandao kote ulimwenguni ambapo wadukuzi hufaidika.

Kazi hizo ni pamoja na operesheni za fidia kwa njia ya mtandao dhidi ya makampuni binafsi ambayo yanalazimishwa kulipa mamilioni kwa madai ya fidia ili kupata tena takwimu zao kulingana na maafisa wa Marekani.

Marekani na nchi kote duniani, zinaiwajibisha Jamhuri ya watu wa China (PRC), kwa mtindo wake wa tabia isiyo ya uwajibikaji, usumbufu katika mtandao wa wavuti ambao unaleta tishio kubwa kwa usalama wetu wa kiuchumi na kitaifa, ilisema taatifa kutoka waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken.

Marekani pamoja na NATO, jumuiya ya ulaya, Uingereza, Japan, Canada, Australia na New Zealand, Jumatatu waliilaumu china kwa shambulizi la mtandao hapo Machi ambalo liliathiri makumi ya maelfu ya taasisi kupitia seva ya Microsoft Exchange.

XS
SM
MD
LG