Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Februari 08, 2025 Local time: 18:09

Hatimaye Hungary yaidhinisha Sweden kujiunga rasmi na NATO


Swedish PM Kristersson and Hungarian PM Orban hoWaziri Mkuu wa Sweden Kristersson na Waziri Mkuu wa Hungary Orban wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari, mjini Budapest.
Swedish PM Kristersson and Hungarian PM Orban hoWaziri Mkuu wa Sweden Kristersson na Waziri Mkuu wa Hungary Orban wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari, mjini Budapest.

Sweden inatarajiwa kujiunga rasmi na NATO katika siku au wiki zijazo, baada ya Hungary hatimaye kutoa idhini yake siku ya Jumatatu – mwanachama wa mwisho kufanya hivyo.

Kama anavyoripoti Henry Ridgwesll, wachambuzi wanasema Sweden inaleta uwezo muhimu katika ushirika wa kujihami wa Magharibi.

Mlingoti wa bendera hauna kitu katika makao makuu ya NATO mjini Brussels – ukisubiri kupandisha bendera yenye rangi za Sweden.

Kikwazo cha mwisho kwa uanacham wa Sweden kimemalizwa Jumatatu – pale wabunge wa Hungary walipopiga kura kuidhinisha hatua hiyo, zaidi ya siku 600 baada ya kuwasilisha maombi.

Viktor Orban, Waziri Mkuu wa Hungary anasema: “Ushirikiano wa kijeshi kati ya Sweden na Hungary na kujiunga kwa Sweden katika NATO kutaimarisha ulinzi wa Hungary.”

Hungary ilikuwa mwanachama wa mwisho wa NATO yenye mataifa 31 kuidhinisha maombi ya Sweden…..

… ambapo Sweden pamoja na Finland waliwasilisha maombi Mei mwaka 2022, miezi mitatu baada ya uvamizi kamili wa Russia nchini Ukraine.

Orban alichelewesha upigaji kura juu ya ukosoaji wa Sweden wa kushuka kwa demokrasia nchini Hungary. Lakini ziara ya Waziri Mkuu wa Sweden, Ulf Kristersson huko Budapest siku ya Ijumma – na ununuzi wa Hungary wa ndege nne za kivita za Swedeish Gripen – ulimaliza mivutano. Kristersson alisema ilikuwa ni ‘siku ya historia.’

Sweden ilitaraji kujiunga rasmi katika NATO katika wiki zijazo – na kuvunja sera ya miongo kadhaa ya kutofungamana upande wowote kijeshi.

Robert Dalsjo, Idara ya Utafiti wa Ulinzi ya Sweden amesema: “Kipande cha mwisho cha fumbo kimeanguka panapostahili, na kuonyesha msimamo wa NATO katika eneo zima la Nordic na Baltic. Sweden inapata usalama katika umati wa nchi na kuungwa mkono na uzuiaji wa nyuklia wa Marekani.”

Sweden pia inaingia ikiwa na uwezo wenye thamani wa kijeshi katika ushirika huo.

Robert Dalsjo, Idara ya Utafiti wa Ulinzi ya Sweden alisema: “Tuna jeshi la anga la kisasa, na ndege za Gripen. Tuna nyambizi nzuri sana, hasa zina uwezo mkubwa katika bahari ya Baltic. Tuna jeshi dogo la wana maji lakini lenye teknolojia ya hali ya juu na tuna, katika eneo, tuna uwezo wa Sub-Arctic.”

Latvia, Lithuania na Estonia kwa kiasi kikubwa zinaoneka ni miongoni mwa mataifa wanachama wa NATO walio katika mazingira hatarishi kwa uwezekano wa kushambuliwa na Russia. Kuwa na Finland na Sweden katika ushirika kunaleta kizuizi chenye nguvu, wanasema wachambuzi.

Charly Salonius-Pasternak, Taasisi ya Finland ya Masuala ya Kimataifa alisema:

“Kuwezesha ulinzi wa Latvia, Lithuani na Estonia kutoka maeneo tofauti. Itakuwa ni uwezekano wa kufanya makubwa zaidi, ukichanganya, operesheni za anga zikiangalia kila upande kuanzia kaskazini huko Finland, na kaskazini magharibi na magharibu huko Sweden, nchi zote mbili ni wanachama wa NATO, kitu ambacho kilikuwa hakikuwezekana kupanga hivyo mwaka mmoja tu uliopita.”

Sherehe ya kujiunga inatarajiwa kufanyika katika siku zijazo baada ya mchakato rasmi kukamilishwa Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg amesema Jumatatu kwamba kujiunga kwa Sweden “kutatufanya sote kuwa wenye nguvu na salama.”

Russia haikujibu haraka. Katika siku zilizopita, ilisema kwamba uanachama wa NATO utaifanya Sweden “lengo halali kwa hatua za majibu za Russia.”

Forum

XS
SM
MD
LG