Hii ni kulingana na ripoti ya shirika la kimataifa la kufuatilia demokrasia iliyotolewa leo Alhamisi.
Kulingana na ripoti hiyo, baadhi ya nchi ambazo zimekuwa zikitambuliwa kuheshimu demokrasia, pia zimejiunga katika orodha ya nchi ambazo viwango vya demokrasia vimeshuka.
Taasisi ya demokrasia na msaada wa uchaguzi IDEA, yenye makao yako Stockholm, Sweden, imesema kwamba viwango vya demokrasia katika nchi 85 kati ya 173 zilizohusishwa katika utafiti huo vimeshuka katika muda wa miaka 5 iliyopita.
Ubaguzi nchini Marekani, ukandamizaji wa uhuru wa waandishi wa habari nchini Austria, na upatikanaji wa haki nchini Uingereza ni miongoni mwa mambo ambayo yametajwa kushuka katika utafiti huo.
Viwango vya demokrasia pia vimeshuka Hungary, Peru na nchi za Afrika ambapo viwango hivyo vimeshuka sana kutokana na mapinduzi ya kijeshi.
Forum