Walinzi wa pwani wa Taiwan wamesema kwamba boti hiyo iliyokuwa na abiria 34 pamoja na mabaharia iliingiliwa kwa zaidi ya nusu saa wakati ikitembeza watalii kwenye visiwa vya Kinman, karibu na mji wa pwani wa Xiamen, uliopo kusini mwa China lakini unadhibitiwa na Taiwan.
Kuan Bi-ling, mkuu wa Baraza la Shughuli za Masuala ya Baharini la Taiwan amewaambia wanahabari Jumanne akiwa mji mkuu wa Taipei kwamba kitendo hicho cha China kinaathiri hisia za watu pamoja na kuzua taharuki, na ni kinyume cha maslahi ya wakazi wa Mlango wa bahari wa Taiwan, ambao una upana wa kilomita 160 linaloitenga China na Taiwan.
Tukio hilo la Jumatatu limekuja siku moja tu baada ya wavuvi wawili wa China kufa maji kufuatia kuzama kwa boti yao wakati wakiwakimbia walinzi wa pwani wa Taiwan wakiwa kwenye eneo la maji ya Taiwan huko Kinmen. Wenzao wawili walionusurika walikamatwa na kushikiliwa na mamlaka za Taiwan.
Forum