Baada ya karibu miongo minne ya utawala wa kimabavu, Hun Sen alipokeza madaraka kwa mtoto wake wa kiume Huna Manet, Julai mwaka jana, kupitia uchaguzi uliokuwa na upinzani dhaifu.
Wakati huo Hun Sen aliweka dhahiri kwamba licha ya kujiuzulu kwake, bado angeendelea kuwa na ushawishi mkubwa wa kisiasa nchini humo. Baada ya uchaguzi wa Jumapili kumalizika, chama chake tawala cha Cambodia People’s Party, CPP, kilidai kushinda wingi wa viti kwenye baraza la Senate, lenye nguvu nyingi nchini humo.
Msemaji wa chama hicho Sok Eysan, amesema kwamba matokeo ya awali yanaonyesha CPP kikiwa kimepata viti 50 kati ya 58 vilivyoko kwenye baraza hilo. Amedhibitisha kwamba chama hicho kitamteua Hun Sen, kama rais wake, na kwa hivyo kumpa nafasi ya kushikilia uongozi wa nchi, pale mfalme anapofanya ziara za nje.
Hilo linatarajiwa kufanyika Aprili pale chama hicho kitakapo kuwa na kikao.
Forum