Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 07, 2024 Local time: 09:32

Kiongozi wa upinzani wa Tunisia aanza mgomo wa kususia chakula akiwa jela


Kiongozi wa upinzani wa Tunisia Rached Ghannouchi.
Kiongozi wa upinzani wa Tunisia Rached Ghannouchi.

Kiongozi wa upinzani wa Tunisia aliye kizuizini Rached Ghannouchi  Jumatatu ameanza mgomo wa chakula, akiwa na wapinzani wengine wa serikali, kama njia ya kushinikiza kuachiliwa kwao, mawakili wao wamesema. 

Ghannouchi mwenye umri wa miaka 82, na ambaye mkosoaji mkubwa wa rais Kais Saied, na pia kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha Ennahda, alifungwa jela mwaka jana kwa tuhuma za kusababisha uchochezi dhidi ya polisi, pamoja na kupanga kuhujumu usalama wa taifa.

Mapema mwezi huu kwenye kesi tofauti, Jaji mmoja alimpatia kifungo cha miaka 3 jela kwa tuhuma kwamba alipokea ufadhili wa fedha wa kigeni. Viongozi 6 wa upinzani waliokamatwa kwenye msako mwaka jana nchini humo, wiki iliopita walianza mgomo wa kususia chakula, wakati wakiwa jela bila kusikilizwa mahakamani, wakiomba kuachiliwa mara moja.

Viongozi hao wameomba kusitishwa kwa ukandamizaji wa mahakama dhidi ya wanasiasa, wanahabari pamoja na wanaharakati wa haki za kiraia.

Forum

XS
SM
MD
LG