Jumatatu, Israel ilisitisha ziara ya wajumbe wake kupinga uamuzi wa Marekani wa kukata kupiga kura ya turufu dhidi ya azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa ambalo liliomba sitisho la mapigano la mara moja katika vita kati ya Israel na Hamas.
Marekani, mshirika mkubwa wa Israel katika vita hivyo vya karibu miezi sita, ilijizuia kupigia kura azimio hilo wiki hii baada ya kupiga kura ya turufu dhidi ya maazimio mengine kama hayo awali. Msimamo huo ulikosolewa na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, na kudhihirisha kuongezeka kwa mgawanyiko na Washington juu ya mwenendo wa serikali hiyo ya Kiyahudi katika vita hivyo.
Licha ya Netanyahu kusitisha ziara ya wataalam hao wa kivita, waziri wa ulinzi wa Israel Yoav Gallant alikuwa Washington wiki hii kwa mazungumzo na waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin na waziri wa mambo ya nje Antony Blinken.
Netanyahu alisema kuishambulia Rafah ni muhimu ili kumaliza udhibiti wa Hamas huko Gaza. Lakini Marekani iliiambia Israel kwamba haikubaliani na uvamizi wa Rafah, haswa kwa sababu zaidi ya Wapalestina milioni 1 wanaishi katika makambi huko.
Forum