Maafisa wa usalama wa taifa na vyombo vya sheria wamekuwa na wasiwasi kwa muda mrefu kuhusu makundi madogo au watu binafsi kushawishiwa na njama za ugaidi duniani kote kufanya mashambulizi nchini Marekani.
Lakini mkurengezi wa idara ya upelelezi FBI, Christopher Wray aliwambia wabunge Alhamisi kwamba jambo la kutisha zaidi linaweza kutokea.
“Jambo linalotia wasiwasi zaidi ni uwezekano wa shambulio lililopangwa kufanyika hapa nchini, sawa na shambulio la ISIS-K tuliloona kwenye jumba la tamasha la Russia wiki chache zilizopita,” Wray aliwaonya wabunge.
Siku chache zilizopita, idara za polisi kote barani Ulaya ziliimarisha usalama baada ya vyombo vya habari vyenye uhusiano na Islamic State, kuchapisha jumbe za kushambulia viwanja vinavyoandaa mechi za ligi ya mabingwa barani Ulaya wiki hii huko Madrid, London na Paris.
Forum