Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 14, 2024 Local time: 10:15

Mashirika makubwa ya ndege yarejesha safari za Mashariki ya Kati


Ndege ya shirika la ndege la Qatar
Ndege ya shirika la ndege la Qatar

Mashirika makubwa ya ndege katika eneo la Mashariki ya Kati yalitangaza kuwa yanaanza tena safari zao katika eneo hilo baada ya kuziahirisha au kubadilisha baadhi, wakati Iran iliporusha dazani za ndege zisizo na rubani na makombora dhidi ya Israel.

Msemaji wa shirika la ndege la Emirates alisema kuwa kufikia Jumapili mchana, shirika hilo la ndege lilikuwa likirejesha ratiba zake za safari za kwenda na kutoka Iraq, Jordan na Lebanon.

Shirika hilo kubwa zaidi katika Mashariki ya Kati, lilikuwa limefuta baadhi ya safari zake za ndege baada ya nchi nyingi za eneo hilo kufunga anga kwa muda, kufuatia mashambulizi ya Iran dhidi ya Israel.

Qatar Airways pia ilirejesha ratiba zake za safari za ndege huko Amman, Baghdad na Beirut, ilisema katika ujumbe kupitia mtandao wa X. Shirika la Ndege la Etihad lenye makao yake makuu mjini Abu Dhabi lilitangaza kuwa litaanzisha upya safari zake za abiria na mizigo kati ya Abu Dhabi na Tel Aviv, Amman na Beirut leo Jumatatu.

Ilitahadharisha, hata hivyo, kwamba kufungwa kwa anga ya nchi za kikanda mwishoni mwa juma kumechangia usumbufu wa huduma na kwamba huenda likatoa huduma zake Jumatatu kwa uwezo mdogo zaidi.

Forum

XS
SM
MD
LG