Mashambulizi mapya ya Ijumaa yalilenga kituo cha nishati katika mkoa wa kusini wa Dnipropetrovsk, ambacho kimepata uharibifu mkubwa baada ya kushika moto kutokana na shambulizi la droni la mapema leo, jeshi la Ukraine na afisa wa mkoa wamesema.
Mkuu wa mkoa huo Serhiy Lysak amesema kuwa wafanyakazi wa zima moto wa Ukraine walifanikiwa kuuzima moto huo, ingawa kiwango cha uharibifu hakikuweza kukadiriwa mara moja. Wakati huo mkuu wa mkoa wa Kherson, Oleksandr Prokudin amesema kuwa mashambulizi ya usiku kucha ya Russia katika mkoa wa kusini mwa Ukraine yameharibu miunjdo mbinu ya kiwanda muhimu ambacho hakijatajwa.
Prokudin amesema kwamba maeneo 15 ya makazi kwenye mkoa huo pia yalishambuliwa, lakini hakuna vifo vilivyo ripotiwa ingawa nyumba kadhaa ziliharibiwa. Ripoti zimesema kwamba mifumo ya ulinzi wa anga ya Ukraine imetungua droni 16 kati ya 17 zilizorushwa na Russia katika mikoa sita, jeshi la Ukraine limesema mapema kupitia ujumbe kwenye mitandao ya kijamii.
Forum