Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 00:31

Israeli yasema vitisho vya Iran havitaizuia kujibu mashambulizi ya wikendi


Mabaki ya kombora ambalo Israeli inasema lilikuwa limerushwa na Iran na kuanguka kwenye bahari ya Dead Sea.
Mabaki ya kombora ambalo Israeli inasema lilikuwa limerushwa na Iran na kuanguka kwenye bahari ya Dead Sea.

Waziri wa Ulinzi wa Israel alisema Jumanne vitisho vya Iran havitazuia taifa lake kujibu mashambulizi ya anga ya Jumapili dhidi ya taifa hilo la Kiyahudi.

Ikirejelea maoni yaliyotolewa na Yoav Gallant katika ziara yake kaskazini mwa Israel, Wizara ya Ulinzi ilimnukuu akisema, "Wairani walishindwa katika shambulio lao na watashindwa kuizuia Israel kutekeleza mpango wake."

Maafisa wakuu wa Marekani wamesema shambulizi la Iran dhidi ya Israel, la kwanza la aina hiyo kutoka ardhi ya Iran, lilihusisha zaidi ya makombora 110 ya masafa marefu, 30 ya mwendo kasi, na zaidi ya 150 ya ndege zisizo na rubani. Walisema vikosi vya washirika wa Iran nchini Iraq, Syria na Yemen pia vilishiriki katika shambulio hilo.

Maafisa wa Iran wametoa onyo za maneno kwa Israel inapotafakari majibu yake, na kuapa kwamba Tehran itajibu haraka na kwa ukali, hatua ya Israel ambayo inadhuru maslahi ya jamhuri hiyo ya Kiislamu.

Forum

XS
SM
MD
LG