Wademokrat walisema kifungu hicho, ambacho kilimshtaki Mayorkas kwa "kukataa kwa makusudi na kwa utaratibu kufuata sheria" ni kinyume cha katiba.
Kiongozi wa Wengi katika Seneti Chuck Schumer, alisema vifungu vya mashtaka dhidi ya Mayorkas "vimeshindwa kufikia kigezo cha uhalifu wa mkubwa na makosa."
Baraza la wawakilishi lilipitisha mswada wa kumshtaki Mayorkas, kwa kura chache mnamo mwezi Februari, uliomtuhumu kwamba alikataa kutekeleza sheria za uhamiaji.
Mayorkas amesema anatilia maanani kazi ya wizara yake. Katika duru ya kwanza ya kura ya Jumatano, maseneta 51 walipiga Kura ya kupinga mashtaka hayo, huku 48 wakiiunga mkono.
51 walipinga katika duru ya pili huku 49 wakiunga mkono.
Forum