Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF Jumatatu limeonya kuwa uamuzi wa Israel wa kuzuia upelekaji wa misaada ya kibinadamu isipokuwa maji kwenye Ukanda wa Gaza, kwa haraka utapelekea hatari kubwa kwa watoto na familia ambazo tayari zimetatizika.
Kampuni kubwa ya kutengeneza chips za kompyuta ya Taiwan Semiconductor Manufacturing, au TSMC Jumatatu imetangaza kuongeza uwekezaji wa dola bilioni 100 hapa Marekani kwa kujenga viwanda 5 zaidi vya kutengeneza chips ndani ya miaka kadhaa ijayo.
Rais wa Marekani Donald Trump amesema Jumatatu kwamba hakuna matumaini kwamba Mexico na Canada wataepuka ushuru wa asilimia 25 unaoanza kutozwa le Jumanne, na hivyo kulitikisa soko la fedha kutokana na vizingiti vipya vya biashara na Marekani.
Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Iran Mohammad Javad Zarif, ambaye alikuwa na nafasi muhimu katika majadiliano ya makubaliano ya kihistoria ya nyuklia ya mwaka 2015, kati ya Iran na mataifa yenye nguvu duniani, amejiuzulu kama makamu wa rais, vyombo vya habari vya serikali vilisema Jumatatu.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amesema kwamba nchi yake iko tayari kutia saini mkataba wa madini nyeti na Marekani, na kwamba anaamini kuwa anaweza kuokoa uhusiano uliodorora kati yake na Rais Donald Trump.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Badir Abdelatty amesema Jumapili kwamba mpango wa kuikarabati Gaza utakaohakikisha kwamba Wapalestina wanabaki kwenye ardhi yao umekamilika na utawasilishwa kwenye mkutano wa dharura wa mataifa ya Kiarabu Jumanne mjini Cairo.
Hali ya vita vya Russia dhidi ya Ukraine vilivyodumu miaka 3 ilibaki kuwa ya wasiwasi Jumapili wakati Marekani ikisema kwamba haina uhakika amani inaweza kupatikana
Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau Jumapili amesema kwamba atazungumza na Mfalme Charles wa Uingereza hukusu kulindwa kwa utaifa wa Canada baada ya tishio la mara kwa mara kutoka kwa rais wa Marekani Donald Trump kwamba itafanywa kuwa jimbo la 51 la Marekani.
Mkutano uliofanyika White House kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy Ijumaa uliolenga kufikia makubaliano ambayo huenda yatairuhusu Marekani kupata haki ya madini nadra ya Ukraine uligeuka kuwa ni malumbano.
Shirika la serikali ya Marekani linalosimamia vyombo vya habari vinavyorusha matangazo kote duniani, USAGM, Alhamisi limetangaza kuwa mwanahabari aliyegeuka mwanasiasa Kari Lake atajunga na shirika hilo kama mshauri maalum.
Rais wa Marekani Donald Trump alisema kwamba ataweka ushuru wa asilimia 25 kwenye bidhaa kutoka Canada na Mexico wiki ijayo kama alivyopanga hapo awali, akidai kuwa nchi hizo mbili, Jirani za Mrekani, bado hazifanyi vya kutosha kuzuia dawa za kulevya kuingia Marekani.
Rais wa Marekani Donald Trump Jumatano alisema kwamba yeye na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy wataisini mkataba unaoipa Marekani haki ya kupata madini adimu ya Kyiv yenye faida kubwa.
Marekani inasema ubalozi wake wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, unaendelea kufuatilia kwa karibu kesi ya kisheria inayowahusu raia watatu wa Marekani ambao wanakabiliwa na hukumu ya kifo.
Spika wa baraza la wawakilishi la Marekani, Mike Johnson alipata kura za kutosha 217-215, ili kupitisha azimio la bajeti Jumanne usiku.
Serikali kuu ya Somalia na Umoja wa Afrika wamekubaliana kuhusu idadi ya wanajeshi kutoka nchi mbalimbali watakaohudumu katika kikosi kipya cha Umoja wa Afrika kufuatia wiki kadhaa za mtafaruku kati ya Ethiopia na Somalia na pia kati ya Somalia na Burundi.
Wahamiaji zaidi wanaotarajiwa kufukuzwa kutoka nchini Marekani waliwasili katika kituo cha kuwashikilia kwa muda cha Guantanamo Bay, nchini Cuba.
Marekani na Ukraine Jumapili zimesema zinakaribia kufikia makubaliano kwa Kyiv Kuipa Washington Sehemu kubwa ya madini yake nadra kama malipo ya fidia kwa mabilioni ya dola ya zana za kijeshi ambazo Marekani iliipa Ukraine kujihami dhidi ya vita vya Russia.
Kremlin imesema leo Ijumaa rais wa Russia Vladimir Putin yupo tayari kwa mazungumzo ya kumaliza vita nchini Ukraine.
Programu ya Maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNDP, kupitia ripoti mpya ya Alhamisi imesema kuwa huenda ikachukua takriban muongo mmoja kwa Syria kurejea kwenye viwango vya kiuchumi vya kabla ya vita, na kama kasi ndogo ya ukuaji iliyopo itaendelea, basi huenda ikachukua zaidi ya miaka 50.
Waziri wa Usalama wa Ndani wa Marekani Kristi Noem Alhamisi amepunguza muda wa kulinda wahamiaji dhidi ya kurejeshwa pamoja na kufuta vibali vya kufanya kazi kwa wahamiaji 521,000 wa Haiti waliokuwa chini ya mpango maalumu ikiwa na maana kwamba utamalizika Agosti, msemaji wa wizara hiyo amesema.
Pandisha zaidi