Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 28, 2025 Local time: 08:10

Misri yasema mpango wa kukarabati Gaza umekamilika


Picha ya majengo yaliyoporomoka Jabalia kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, March 1, 2025.
Picha ya majengo yaliyoporomoka Jabalia kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, March 1, 2025.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Badir Abdelatty amesema Jumapili kwamba mpango wa kuikarabati Gaza utakaohakikisha kwamba Wapalestina wanabaki kwenye ardhi yao umekamilika na utawasilishwa kwenye mkutano wa dharura wa mataifa ya Kiarabu Jumanne mjini Cairo.

Mataifa ya Kiarabu, ambayo kwa haraka yalipinga mpango wa Rais Donald Trump kwa Marekani kuchukua udhibiti wa Gaza na kuwahamisha Wapalestina, yanajitahidi kuafikiana kuhusu hatua za kidiplomasia ya kukabiliana na wazo hilo.

Mpango wa Trump ulitangazwa Februari 4 wakati kukiwa na sitisho tete la mapigano kati ya Israel na kundi la Hamas, ambalo Marekani imelitajia ni kundi la kigaidi, ukionekana kwenda kinyume na sera ya muda mrefu ya Marekani kwa Mashariki ya Kati, ya kuundwa kwa mataifa mawili, na hivyo kuchochea ghadhabu miongoni mwa Wapalestina na mataifa ya Kiarabu.

Abdelatty amesema Misri itatafuta uungaji mkono wa kimataifa na ufadhili kwa mpango na kusisitiza jukumu muhimu la Ulaya, hasa katika kufadhili ujenzi tena wa Gaza. Israel Jumapili ilifunga njia muhimu kwa malori ya misaada kuingia Gaza wakati kukiwa na hali ya sintofahamu kuhusu sitisho la mapigano ambalo limekuwepo kwa wiki 6 sasa. Duru ya kwanza ya sitisho hilo imemalizika mwishoni mwa wiki.

Forum

XS
SM
MD
LG