"Barua ya kujiuzulu ya Zarif ilipokelewa na Rais Masoud Pezeshkian, ambaye bado hajajibu," shirika rasmi la habari la IRNA liliripoti, bila kutoa maelezo zaidi.
Katika ujumbe wa Jumatatu kwenye mtandao wa kijamii wa X, Zarif alisema "amekabiliwa na matusi ya kutisha, shutuma na vitisho dhidi yake na familia yake, na kwamba amepitia kipindi kigumu zaidi cha miaka yake 40 ya utumishi wa umma.
"Ili kuepuka shinikizo zaidi kwa serikali, mkuu wa mahakama alipendekeza nijiuzulu na... nilikubali mara moja," aliongeza.
Pezeshkian, ambaye aliingia madarakani mwezi Julai, alimteua Zarif kama makamu wake wa rais kwa masuala ya kimkakati mnamo Agosti 1 lakini Zarif alijiuzulu baada ya chini ya wiki mbili, kabla ya kurejea katika wadhifa huo baadaye mwezi huo.
Zarif alikuwa mwanadiplomasia mkuu wa Iran kati ya mwaka 2013 na 2021 katika serikali ya rais mwenye msimamo wa wastani, Hassan Rouhani.
Forum