Hali limejiri wakati viongozi wa Ulaya wakisisitiza uungaji mkono wao kwa majeshi ya Kyiv, na kuapa kuongeza matumizi yao ya ulinzi pamoja na kutuma walinda usalama kufanya doria iwapo litapatikana kwa mzozo huo.
Siku mbili baada ya rais wa Marekani Donald Trump alimbeza rais wa Ukraine Volodymr Zelenskyy wakati wa ziara yake hapa Marekani kwamba hana shukrani kwa msaada wa kijeshi wa Marekani na kwamba anaonekana kutokuwa “tayari” kwa amani, Waziri Mkuu wa Uingereza Kier Starmer aliwaambia washirika 18 mkutano wa London kwamba wakati Marekani ikionekana kuyumba yumba kwenye uungaji mkono wake kwa Kyiv, Ulaya inajikuta “iko kwenye njia panda katika historia”.
“Huu si wakati wa mazungumzo zaidi, ni wakati wa kuchukua hatua. Ni wakati wa kuongeza juhudi, kuongoza na kuungana kwenye mpango mpya wenye haki kuelekea amani ya kudumu,” alisema Starmer. Wakati huo huo mshauri wa Usalama wa Taifa wa Trump, Michael Waltz, alipokuwa akizungumza kuhusu Zelenskyy Jumapili alikiambia kituo cha televisheni cha CNN katika kipindi cha “State of The Union” kwamba,
“Kile ambacho hakikuwa dhahiri kwetu ni akama alikuwa na lengo kama letu la kumaliza vita hivi. Haikuwa wazi alikuwa tayari kwa amani.”
Forum