Hatua hii ni kuendeleza juhudi za chama cha Republican za kuongeza muda wa ziada wa kulipa kodi na kupunguza matumizi ambayo Wademokrat wameyaita yasiyo na msingi.
Johnson na viongozi wa Warepublikan kwenye Baraza la Wawakilishi wamesema katika taarifa kuwa lengo lao ni mswada wa kulinda mpaka, kupunguza kodi kwa familia na wazalishaji wa ajira, kurejesha utawala wa nishati wa Marekani.
Pia ni kuimarisha msimamo wa Marekani ulimwenguni, huku serikali ikifanyakazi kwa ufanisi zaidi.
Spika Johnson alieleza kuwa: “Tuna kazi ngumu sana mbele yetu, lakini tutawasilisha ajenda ya Marekani Kwanza. Tutawasilisha yote, sio baadhi ya sehemu zake tu. Hii ni hatua ya kwanza katika mchakato huo.”
Rais Donald Trump ametoa wito kwa wabunge kupitisha mswada anaouita “mkubwa na mzuri” ambao utakuwa sehemu muhimu ya kutekeleza ajenda zake katika sera ya mambo ya ndani.
Forum