Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilikataa kutoa maoni yake kama kuna mazungumzo yanayo endelea ili kuachiliwa kwa Wamarekani hao.
Mwishoni mwa wiki, mjumbe maalum wa Rais wa Marekani, anaye shughulikia mateka, Adam Boehler, aliandika katika mtandao wa kijamii kwamba Wamarekani hao watatu bado wanashikiliwa na serikali ya DRC.
Septemba 2024, mahakama ya kijeshi nchini DRC iliwahukumu kifo watu 37, wakiwemo Wamarekani watatu Tyler Thompson Jr., Marcel Malanga na Benjamin Reuben Zalman Polun kwa jaribio la mapinduzi yaliyoshindikana hapo Mei 2024.
Forum