“Kusitishwa kwa upelekaji wa misaada kulikotangazwa Jumapili kutaathiri pakubwa operesheni za raia,” amesema Eduoard Beigbeder, mratibu wa kieneo wa UNICEF kwa ajili ya Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika.
“ Ni muhimu kwa sitisho la mapigano kuendelea kuwepo, pamoja na kuruhusiwa kwa upelekaji wa misaada ili tuweze kuendelea na shughuli za kibinadamu,” Beigbeder amesema. Jumapili Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema kuwa mjumbe maalum wa Marekani kwa ajili ya Mashariki ya Kati Steven Witkoff alipendekeza kuongezwa kwa muda wa sitisho la mapigano hadi Aprili 20.
Tarehe hiyo itatoa nafasi kwa mwezi mtukufu wa Ramadan pamoja na siku kuu muhimu ya Wayahudi ya Pasaka. Ndani ya kipindi hicho, Hamas wataachilia nusu ya mateka waliyoshikiliwa na kisha kuachilia waliyobaki pale sitisho la kudumu la mapigano litakapofikiwa. “ Nimekubaliana na mpango huo ingwa kufikia sasa Hamas wameukataa,” Netanyahu alisema kupitia ujumbe wa video.
Forum