“Ni lazima watozwe ushuru. La sivyo watalazimika kutengeneza viwanda vyao vya magari kwa kweli na vingine ndani ya Marekani ili kuepuka kulipa ushuru,” Trump alisema akiwa White House.
Trump pia alisema kwamba majibu ya ushuru huo yataanza kufanya kazi Aprili 2 kwa nchi zitakazoweka ushuru kwa bidhaa za Marekani. Thamani ya hisa kwenye soko la Marekani ilishuka muda mfupi baada ya matamshi ya Trump. Wakuu wa makampuni pamoja na wataalam wa kiuchumi wamesema kwamba hatua hiyo itaathiri biashara ya zaidi ya dola bilioni 900 kila mwaka kutokana na bidhaa ambazo huingia Marekani kutoka Canada na Mexico, na pia kuathiri soko la pamoja na Marekani Kaskazini.
Waziri wa mambo ya nje wa Canada Melanie Joly wakati akizungumza na wanahabari alisema kuwa Ottawa ipo tayari kujibu. Akizungumza na CNN, Waziri wa Biashara wa Marekani Howard Lutnick alisema kwamba Canada na Mexico walikuwa wamepiga hatua kuimarisha usalama mipakani, lakini juhudi zinahitaji kuongezwa ili kuzuia uingizaji wa dawa za kulevya za fentanyl ndani ya Marekani ili kupunguza vifo miongoni mwa watumiaji.
Forum