Matamshi ya Trump yamewaghadhabisha wengi nchini Canada, wakati maafisa wakipinga vikali uwezekano wa mashauriano ya aina yoyote ile ya kuifanya Canada kuwa sehemu ya Marekani.
Wakati akikutana na Mfalme Charles ambaye ndiye kiongozi wa taifa la Canada Jumanne, Trudeau alisema kuwa wangezungumzia maswala muhimu ya Canada pamoja na watu wake.
Tangu kuingia madarakani mwaka huu, Trump amekuwa akiitaja Canada mara kwa mara kama jimbo la 51 la Marekani na hata kumuita Waziri Mkuu Trudeau, Gavana.
Trump ameamuru ushuru uwekwe dhidi ya mshirika mkuu wa kibiashara wa Marekani, na vinapangwa kuanza Jumanne, wakati akisema huenda hilo linaweza kuepukika kama Canada itakuwa sehemu ya Marekani.
Mwezi uliopita, Trudeau alionya kuwa tishio la Trump la mara kwa mara kuhusu kuichukua Canada ili kufikia rasilimali zake asili “ni suala la kweli.”Baadhi ya raia wa Canada wanasema kwamba hawaelewi kwanini Mfalme Charles hajazungumza kuitetea Canada.
Forum