Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo C.C.Wei, alitangaza mpango huo wakati wa kikao huko White House na Rais wa Marekani Donald Trump. “ Ni lazima tuweze kutengeneza chips na semiconductor tunazohitaji hapa ndani ya nchi,” Trump alisema. “Ni suala la usalama wa taifa kwetu sisi.”
Kampuni ya TSMC ni kubwa zaidi duniani kwenye utengenezaji wa vidude vya kompyuta, soko lake kubwa likiwa hapa Marekani. Ushindi kwenye uchaguzi wa Novemba ukichochewa zaidi na matumaini ya kiuchumi kwa wapiga kura, Trump amejitahidi kuinua uwekezaji kwenye viwanda vya ndani ili kubuni ajira.
Tangazo la uwekezaji wa TSMC ni moja wapo ya mengine yaliyofanywa katika siku za karibuni. Mwezi uliopita, kampuni ya Apple ilitangaza uwekezaji wa dola bilioni 500 ndani ya kipindi cha miaka minne ijayo. Bilionea wa Emirati Hussain Sajwani pamoja na SoftBank pia wameahidi kuwekeza mabilioni ya dola hapa Marekani.
Forum