Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 23:35

Wapalestina wakusanyika Gaza kuukumbusha ulimwengu haki ya ardhi yao


Wapalestina wakiwa wamebeba mwili wa Mpalestina aliyeuawa katika eneo la mpaka kati ya Israeli-Gaza, ndani ya hospitali ya mji wa Gaza Machi 30, 2019.
Wapalestina wakiwa wamebeba mwili wa Mpalestina aliyeuawa katika eneo la mpaka kati ya Israeli-Gaza, ndani ya hospitali ya mji wa Gaza Machi 30, 2019.

Maelfu ya Wapalestina wamekusanyika katika eneo la mpakani kati ya Gaza na Israeli Jumamosi kuadhimisha mwaka wa kwanza wa wimbi la maandamano ya kukumbusha ulimwengu juu ya haki ya ardhi yao, na kuvikabali vikosi vya Israeli vilivyokuwa vimekusanyika mpakani.

Vikosi hivyo vya Israeli vilitupa mabomu ya machozi kuwatawanya Wapalestina waliokuwa mpakani hapo na jeshi la Israeli limesema inakadiriwa kuwa takriban waandamanaji 20,000 walikuwa wakitupa mawe, maguruneti na kusukuma matairi yanayowaka moto kuelekea kwa vikosi hivyo.

Wanaharakati wa Palestina wakiwa wamevalia vizbao rangi ya machungwa walikuwa wakijaribu kuwazuia waandamanaji, japokuwa baadhi yao walifanikiwa kufikia uzio ulioko mpakani.

Ghasia zimeshuhudiwa katika eneo la mpaka wa Israeli na Gaza wiki hii kabla ya kufanyika maandamano ya kumbukumbu yanayojulikana kama 'Great March of Return' (Maandamano ya Wapalestina kurejea katika ardhi yao) yaliyoanza Machi 30, 2018.

Risasi iliyotupwa kutoka jeshi la Israeli ilimuuwa mwanaume wa Kipalestina aliyekuwa karibu na Ukanda wa Gaza Jumamosi, maafisa wa afya wamesema.

Wakati huohou, majeshi ya Israeli yameendelea kukusanyika mpakani kabla ya mkusanyiko (Great March of Return) uliopangwa kuadhimisha mwaka wa kwanza wa msukumo mkubwa wa maandamano hayo kwenye mpaka wa Gaza.

Takriban wananchi wa Gaza 200 wameuawa na vikosi vya Israeli tangu maandamano hayo yaanze, kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Afya ya Palestina, na askari wa Israeli aliuawa na Mpalestina aliyepiga bunduki kutoka mafichoni.

Wapalestina wanapaza sauti wakishinikiza kuondolewa kizuizi cha usalama kilichowekwa na Israeli na Misri, na wanataka Wapalestina kuwa na haki kurejea katika ardhi yao ambayo familia zao zililazimika kuikimbia au kulazimishwa kukimbia wakati taifa la Israeli lilipoundwa mwaka 1948.

Jeshi la Israeli limesema kuwa lilikuwa halijapata taarifa juu ya tukio hilo. Madaktari wa Palestina wamesema mtu huyo aliuawa kwa risasi kabla ya alfajiri katika eneo ambako mara nyingi maandamano yanafanyika karibu na mpakani.

Siku ya Ijumaa usiku, jeshi la Israeli lilisema kuwa Wapalestina walikuwa wakirusha vilipuzi katika uzio ulioko mpakani.

Zaidi ya Wapalestina milioni 2 wamejazana katika eneo finyu lililotengwa la pwani ambapo umaskini na ukosefu wa ajira uko katika viwango vya juu.

Vizuizi hivyo vilivyowekwa na Israeli vinaelezewa na mashirika ya kibinadamu ni sababu kuu ya umaskini katika ukanda wa Gaza.

Mapigano yalizuka wakati Wapalestina walipotupa roketi shambulizi kutoka Gaza lilowajeruhi Waisraeli saba katika Kijiji kilichopo kaskazini ya Tel Aviv, Jumatatu. Katika kujibu mashambulizi hayo, Israeli ilifanya mashambulizi kadhaa ya angani na kusogeza vifaa vyake vya kijeshi na majeshi ya ziada katika mpaka wake.

Majeshi ya Israeli yamebakia katika eneo la mpakani hadi Jumamosi, na jeshi limesema linatarajia kuwepo “machafuko ya uvunjifu wa amani” na ilikuwa tayari imejitayarisha kwa kuongezeka hali hiyo ya hatari.

Maelfu ya wananchi wa Palestina walikuwa wanatarajiwa kuandamana, ambapo maandamano hayo yamekuwa ni hatari kubwa katika siku za nyuma, na wasuluhishi wa Misri wamekuwa wakijitahidi kuzuia kumwagika damu zaidi.

Viongozi wa makundi yenye silaha ya Hamas na Islamic Jihad ndani ya Gaza wamesema mazungumzo ya kutafuta suluhu yanaendelea kuonyesha mafanikio.

XS
SM
MD
LG