Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 22:26

Trump afanya ziara yake ya kwanza Israeli


Rais Donald Trump na Mkewe wakiwasili Isreali
Rais Donald Trump na Mkewe wakiwasili Isreali

Rais Donald Trump amewasili Jumatatu Israeli, ikiwa ni ziara yake ya mara ya kwanza tangu awe rais ambaye ana azma ya kufufua juhudi za kufikia makubaliano ya amani kati ya Israeli and Palestina.

Katika safari yake hiyo Ndege yake ya Air Force One imefanya safari ya kihistoria bila ya kusimama popote kati ya Riyadh na Tel Aviv Jumatatu.

Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu na Rais Reuven Rivlin walikuwa katika umati wa watu waliojitokeza katika hafla ya kumpokea Trump uwanja wa ndege wa Ben-Gurion.

Kabla ya kuondoka Riyadh Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson alikuwa amepangiwa kuzungumza na waandishi akiwa katika ndege ya Air Force One wakati wa safari hiyo, kwa mujibu wa ikulu ya White House.

Hii inafuatia mabadiliko ya Jumapili wakati alipozungumza na waandishi wa kigeni mjini Riyadh akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia Adel al-Jubeir.

Waandishi wa Rais wanaosafiri naye walikuwa hawajapewa taarifa mapema kuhusu mkutano huo wa waandishi wa habari.

Rais Donald Trump anafanya ziara yake ya kwanza Israeli akiwa rais ambaye anataka kurejesha juhudi ya kufikia makubaliano ya amani ambayo yamekuwa yakifanyiwa kazi kwa muda mrefu kati ya Israeli na Palestina.

Ratiba ya Trump inaonyesha atafanya mikutano na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu na Rais wa Palestina Mahmoud Abbas, na Trump anatarajiwa kuwa rais wa kwanza aliyeko madarakani kutembelea sehemu takatifu ya dini ya Uyahudi (Judaism), ukuta maarufu wa Western Wall.

Machi mwaka huu, Trump alisema kuwa pengine “sio vigumu kama watu wanavyofikiria” kufikia amani kati ya Israeli na Palestina, lakini hajatoa kielelezo chochote jinsi atavyoweza kukabiliana na suala hilo tofauti na vile viongozi wenzake waliopita walivyokuwa wakifanya. Amemuamrisha mkwe wake na mshauri wa ngazi ya juu Jared Kushner kuongoza juhudi hizo kwa niaba ya White House.

Trump alisema wakati wa kampeni ya urais kuwa njia bora zaidi ya mazungumzo kufikia makubaliano kati ya pande mbili hizo ni kuchukua kile alichokiita mwenendo usiofungamana na upande wowote katika masuala nyeti na yenye hamasa na kuhakikasha pande zote mbili zinakaa kando.

Lakini pia amesema kuendelea na ujenzi wa makazi ya Israeli haitosaidia katika mchakato wa amani, na amesitisha ahadi yake ya kuuhamisha Ubalozi wa Marekani kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalem.

XS
SM
MD
LG