Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 01:53

Ubalozi wa Marekani wahamia Jerusalem


Maafisa wa usalama wakiimarisha ulinzi katika njia inayoelekea ubalozi wa Marekani huko Jerusalem, Mei 13, 2018.
Maafisa wa usalama wakiimarisha ulinzi katika njia inayoelekea ubalozi wa Marekani huko Jerusalem, Mei 13, 2018.

Marekani imehamisha ubalozi wake kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalem.

Waziri wa Fedha wa Marekani Steven Muchin, amesema Jumatatu kwamba baraza la Congress limekuwa likiunga mkono hatua hiyo kwa Zaidi ya miaka 20.

Ufunguzi huo unafuatia uamuzi wa Rais wa Marekani Donald Trump wa kuitambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel, hatua ambayo imeighadhabisha Palestina na nchi nyingine za Kiislamu.

Ujumbe wa Marekani akiwemo mshauri wa Rais Donald Trump juu ya Mashariki ya Kati, Jared Kushner pamoja na binti ya rais Ivanka Trump ambaye pia ni mshauri wake wanahudhuria ufunguzi huo rasmi wa ubalozi.

Nchi kadhaa za Umoja wa Ulaya zimesusia hafla ya ufunguzi wa ubalozi wa Marekani mjini Jerusalem, lakini zaidi ya nchi 30 kutoka kote duniani zinaunga mkono hatua hiyo.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kwamba Guatemala na Paraguay zitahamishia balozi zao mjini Jerusalem katika siku za hivi karibuni.

Maelfu ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza wamepanga kufanya maandamano makubwa kupinga kuhamishwa kwa ubalozi wa Marekani kutoka Tel Aviv hadi Jerusalem.

Wapalestina wawili wameuawa leo na wengine takriban 93 wamejeruhiwa katika ukanda wa Gaza katika makabiliano na wanajeshi wa Israel.

XS
SM
MD
LG