Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 01, 2024 Local time: 22:59

Trump ampa Netanyahu zawadi kubwa kabla ya uchaguzi Israeli


Rais Donald Trump baada ya kusaini tamko la kuitambua haki ya Israeli kumiliki ardhi ya Golan Heights, huku Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu akishuhudia tukio hilo White House, Washington, Jumatatu, Machi 25, 2019.
Rais Donald Trump baada ya kusaini tamko la kuitambua haki ya Israeli kumiliki ardhi ya Golan Heights, huku Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu akishuhudia tukio hilo White House, Washington, Jumatatu, Machi 25, 2019.

Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu aliyefupisha ziara yake jijini Washington kufuatia shambulizi la roketi kutoka Ukanda wa Gaza, amepokea zawadi kubwa kabla ya uchaguzi kutoka kwa Rais Donald Trump kabla ya kurejea nyumbani siku ya Jumatatu.

Netanyahu akiwa pembeni yake, Trump amesaini amri inayoitambua haki ya Israeli kukalia milima ya Golan Heights.

“Hili lilikuwa ni jambo linaendelea muda mrefu. Ilitakiwa lingefanyika miongo mingi iliyopita,” amesema Rais wa Marekani.

Netanyahu amesema saini ya Trump imegeuza ushindi wa kijeshi wa nchi yake kwa zaidi ya nusu karne iliyopita kuwa ni ushindi wa kidiplomasia.

“Tutaendelea kushikilia milima hiyo na hatutairejesha kamwe,” amesema kiongozi huyo wa Israeli.

Tamko hilo ni lenye kuboresha nguvu ya kisiasa ya Netanyahu ambaye anakabiliwa na kipingamizi kikubwa katika awamu ya pili ya uchaguzi wake kuliko ilivyotarajiwa baada ya polisi mwezi Februari kupendekeza kuwa waziri mkuu anayo mashtaka ya kujibu juu tuhuma za rushwa, ulaghai na kuvunja uaminifu.

Amri ya Trump juu ya Golan Heights “ ni wazi kuwa ni jaribio la kuhakikisha kuwa Netanyahu anachaguliwa kwa gharama yeyote na kwamba bila ya Netanyahu, ushirikiano wa Israel na Marekani hauwezi kuwepo kama ulivyo hivi leo.

Na sitoshangazwa iwapo hili litamsaidia katika uchaguzi, pamoja na kuwa anayo mashtaka ya kujibu,” Zena Agha, mtafiti wa sera za Marekani kwa niaba ya taasisi ya Al-Shabaka, ambayo ni mtandao wa sera ya Palestina, ameiambia VOA.

Syria imeliita tamko la Trump juu ya milima ya Golan Heights kuwa ni shambulizi dhidi ya uhuru na heshima ya ardhi yake.

XS
SM
MD
LG