Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 29, 2022 Local time: 18:50

Netanyahu akataa kujiuzulu kufuatia kashfa ya ufisadi


Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu

Kiongozi ambaye yuko kwenye madaraka kwa muda mrefu sasa amekataa shinikizo la kujiuzulu kwake linalotokana na muendelezo wa kashfa ya ufisadi.

Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu amesema muungano wa serikali yake uko imara, siku moja baada ya polisi kutoa pendekezo la yeye kushtakiwa kwa kesi mbili za ufisadi.

Ameeleza kuwa madai hayo ya ufisadi ni yenye “kumkandamiza, yamevuka mipaka na kuna dosari nyingi kama vile ilivyo jibini ya Uswiz” na kuahidi kuendelea na uongozi wake.

Polisi wametuhumu Netanyahu kwa kupokea rushwa na kukiuka dhamana aliyopewa kwa kumhusisha na kashfa mbili za ufisadi na wanasema kuna ushahidi wa kutosha wa kumfungulia mashtaka.

Wapelelezi wa polisi wamedai kuwa Netanyahu alipokea takriban dola za Marekani 300,000 kama zawadi kutoka kwa mabilionea wawili, zikiwemo aina ya sigara kutoka Cuba “cigars”, ulevi aina ya champagne na mapambo aliyopokea kinyume cha sheria.

Pia imedaiwa kuwa alifikia makubaliano na mchapishaji wa magazeti wa Israel kwa ajili ya kuwataka wachapishe habari chanya juu yake. Na hivyo polisi wanasema kuwa aliahidi kusimamia maslahi yao watakapo msaidia katika kuzuia kashfa hiyo isichapishwe.

Viongozi wa upinzani nchini Israeli wanataka Netanyahu ajiuzulu, wakisema kuwa ni fisadi na hafai kuliongoza taifa.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG