Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 13:56

White House yalaani shambulizi la Iran dhidi ya Israel


Jeshi la Israeli likifanya ulinzi katika eneo la Golan-Heights.
Jeshi la Israeli likifanya ulinzi katika eneo la Golan-Heights.

White House imelaani mashambulizi ya roketi yaliyofanywa na Iran katika eneo linalokaliwa na Israeli –Golan Heights na kuwa halikubaliki na ni hatari kwa maendeleo ya eneo lote la Mashariki ya Kati.”

Katika tamko lililotolewa Alhamisi asubuhi, White House imesema kuwa walinzi wa jeshi la Mapinduzi la Kiislam la Iran (IRGC) “litawajibika kikamilifu kwa matokeo yoyote ya vitendo vyao vya ovyo” na kuonya kuwa jeshi hilo na “wanamgambo wanaopigana kwa niaba yao” wasiendelee kufanya “vitendo vya uchokozi zaidi.”

Israel imesema Alhamisi ndege zake za kivita zilipiga dazeni ya vituo vya kijeshi vya Iran ndani ya Syria usiku wa Jumatano ikiwa ni hatua ya kujibu mashambulizi hayo.

Jeshi la Israeli limesema kuwa shambulizi hilo la anga lililenga vituo vya kijasusi, maghala ya silaha na vituo vya kupanga vita, na kuwa ndege hizo za kivita pia ziliangamiza mifumo ya ulinzi wa anga ya Syria.

Pia Israel imeonya kuwa “haitoruhusu vitisho vya Iran kujikita katika ardhi ya Syria” na wamesema serikali ya Syria itawajibishwa “kwa kila kitu kinachotokea katika ardhi yake.”

XS
SM
MD
LG