Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 28, 2022 Local time: 21:56

Golan Heights : Uamuzi wa Trump waushangaza uongozi wa Mashariki ya Kati


Rais Donald Trump

Hatua yakustaajabisha ya Rais Donald Trump kutambua uhalali wa milima ya Golan Heights kuwa chini ya himaya ya Israeli imezua hisia nzito hasi kutoka kwa Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na viongozi wengine wa Mashariki ya Kati.

Trump alitangaza msimamo wake kupitia ujumbe wa Twitter Alhamisi, akisema eneo hilo ni “ la mkakati na umuhimu mkubwa kwa taifa la Israel na utulivu wa Mashariki ya Kati!”

Tangazo hilo limetolewa saa kadhaa baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo, akiwa katika ziara mjini Jerusalem, alifika katika eneo lenye mvutano ambapo upo ukuta wa Western Wall katika mji mtakatifu wa Jerusalem, akiwa na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu. Pompeo amekuwa ni afisa wa ngazi ya juu kabisa, ambaye pekee hadi sasa amepata fursa ya kufuatana na kiongozi wa Israeli katika eneo hilo lenye utata.

Eneo la Golan Heights – linalokadiriwa kuwa na kilomita za mraba 1,800 lilioko upande wa kaskazini mashariki mwa Israel linalopakana na Syria, lilichukuliwa kwa nguvu na Israeli mwaka 1967 katika vita viliyodumu kwa siku sita.

Baada ya hapo Israeli ilianza rasmi kuikalia kwa mabavu mwaka 1981. Lakini Jumuiya ya Kimataifa haijaitambua Israeli kama mmiliki wa Golan Heights. Tangu wakati huo Israeli imeendelea kulikalia kwa mabavu.

Akizungumza akiwa Istanbul Ijumaa, wakati wa mkutano wa Jumuiya ya muungano wa nchi za Kiislam, Erdogan alichukuwa msimamo tofauti kabisa kufuatia maamuzi ya Trump akisema kuwa hilo litahatarisha eneo la Mashariki ya Kati.

“Tamko la kusikitisha la Rais wa Marekani Donald Trump alilolitoa Alhamisi kuhusu milima ya Golan Heights limeiingiza eneo hilo katika hatari ya kuingia katika mgogoro mpya na mivutano mipya.”

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu amesema uamuzi huo unatukumbusha shambulizi la itikadi za ubaguzi lililotokea wiki iliyopita New Zealand, akisema kuwa matamko ya Rais Donald Trump wa Marekani juu ya Golan Heights hayakubaliki, yanaingia katika fikra kama hizo potofu zinazoweza kuleta hatari.”

Viongozi wengine wa Mashariki ya Kati wamepinga kwa kishindo tangazo hilo pia. Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, Ahmed Aboul Gheit ametupilia mbali tangazo hilo la Trump, akisema “Hakuna nchi, bila ya kujali umuhimu wake, linaweza kufanya uamuzi kama huo.” Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imetoa tamko likisema uamuzi huo “sio makini” na kuwa hazibadilishi “ukweli kuwa Golan ilikuwa na itabaki kuwa ni ya Waarabu na Wananchi wa Syria.”

Netanyahu anatarajiwa kumtembelea Trump huko White House, Washington mapema wiki ijayo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG