Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 21, 2024 Local time: 21:35

Marekani yaitambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israeli


Waziri wa Mambo ya Nje Rex Tillerson
Waziri wa Mambo ya Nje Rex Tillerson

Rais Donald Trump amesema kuwa Marekani inaitambua rasmi Jerusalem kuwa ni Mji Mkuu wa Israel na mara moja mchakato wa kuhamisha ubalozi wake kutoka Tel Aviv umeanza, wakati tukio hilo likikaribisha mvutano hasi kutoka nchi nyingi duniani.

“Jerusalem siyo kwamba tu ni kitovu cha dini kubwa tatu duniani, lakini hivi sasa ni kiini cha demokrasia yenye mafanikio makubwa duniani,” Trump amesema katika hotuba yake Jumatano.

Amesisitiza kuwa Marekani bado imejikita katika kusaidia kurahisisha kupatikana mkataba wa amani ambao unakubalika na pande zote “Israel na Palestina.” Nakusudia kufanya kila ninachoweza katika utawala wangu kusaidia pande mbili kufikia makubaliano,” Trump amesema.

Mapema Jumatano Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson alisema Jumatano kuwa Marekani bado inafikiri kuwa “kuna fursa nzuri sana ya kufikia amani” kati ya Israeli na Palestina huko Mashariki ya Kati.

Amesema licha ya Rais Donald Trump kuwa ameanza kutoa matamko yenye utata kuwa Marekani itautambua mji wa Jerusalem kuwa ni makao makuu ya Isreali bado kuna fursa ya kufikia amani.

Akiwa huko Brussels, Tillerson amesema Trump anania ya kuendeleza mchakato wa mazungumzo ya amani Mashariki ya Kati. Tayari ana timu ambayo ameiuunda.

Timu hiyo imekuwa ikifanya kazi kwa bidii.” Mwanadiplomasia wa juu wa Marekani amehimiza watu “kusikiliza kwa makini hotuba yake yote” aliotoa Trump.

Tangazo linalotegemewa kutolewa na Trump tayari limeibua hisia tofauti kutoka katika nchi za Kiarabu na Kiislam, ambao wamesema uamuzi huo wa kuhamisha Ubalozi wa Marekani kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalem.

Viongozi wengi wameeleza kuwa linaweza kuleta mvutano mkubwa katika eneo la Mashariki ya Kati na kuharibu juhudi za Marekani katika kufikia suluhisho la amani baina ya Israeli na Palestina.

Wapalestina wametangaza kuwa kwa muda wa siku tatu wataonyesha kuudhiwa kwao na uamuzi huo na kuupinga mpango wa Trump.

Rais wa Iran Hassan Rouhani amekosoa uamuzi wa Trump na kusema: “ni kosa, kinyume cha sheria, ni uchochezi na ni hatari kubwa.” Amesema Iran haitovumilia uharibifu wa maeneo matakatifu ya Kiislam. Waislam lazima wasimame pamoja dhidi ya hujuma hii kubwa.”

XS
SM
MD
LG