Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 07:11

Uturuki yapanga kufungua ubalozi Jerusalem mashariki


Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan akizungumza katika mkutano na waandishi Istanbul, Turkey.
Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan akizungumza katika mkutano na waandishi Istanbul, Turkey.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema Jumapili ana matumaini ya kufungua ubalozi wa Uturuki katika taifa la Palestina ndani ya Jerusalem Mashariki

Akizungumza katika hotuba kwenye mkutano wa chama chake katika mji wa Karaman, Erdogan alisema "kwa sababu (Palestina) inakaliwa kimabavu hatuwezi kuingia tu na kufungua ubalozi."

"Lakini, Inshallah, siku hizo zipo karibu, na tutafungua ubalozi huko," alisema, bila kutoa ratiba ya aina yoyote katika hatua hiyo.

Matamshi hayo ya Erdogan yamekuja siku chache tu baada ya Uturuki kufanya mkutano na viongozi wa mataifa yenye waiislamu wengi, kupinga uamuzi wa Rais Donald Trump wa Marekani kuitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel. Erdogan amekuwa akiongoza upinzani wa viongozi wa nchi za kiislamu na Ulaya dhidi ya uamuzi wa Trump.

Jerusalem Mashariki ilitekwa na Israel kufuatia vita vya mwaka 1967 - hatua ambayo haijatambuliwa na jumuiya ya kimataifa.

Uturuki kwa hivi sasa ina ubalozi mdogo Jerusalam, na ina uhusiano kamili wa kibalozi na Israel ikiwa ni pamoja na kuwa na ubalozi kamili mjini Tel Aviv kama ilivyo kwa mataifa mengine duniani.

XS
SM
MD
LG