Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Agosti 14, 2022 Local time: 21:21

Arab League yahofia kuzuka umwagaji damu Mashariki ya Kati


Mawaziri wa nchi za nje wa Umoja wa nchi za Kiarabu walipokutana mjini Cairo, Misri Disemba 9, 2017.

Umoja wa nchi za Kiarabu (Arab League) umesema kuwa uamuzi wa Rais wa Marekani Donald Trump kuitambua Jerusalem kuwa makao makuu ya Israel ni "hatua ya hatari" ambayo inaweze kuleta mgogoro mkubwa Mashariki ya Kati.

Umoja huo umefafanua kuwa uamuzi huo "unaiweka Marekani katika mtazamo wa kuwa inafanya upendeleo kwa wale ambao ni wavamizi na waliokiuka sheria za kimataifa na maazimio yake.”

Tamko hilo limetolewa mapema Jumapili baada ya mkutano wa dharura wa mawaziri wa nchi za nje wa Umoja huo kukutana Cairo na wote kwa pamoja kusema kuwa uamuzi wa Trump pia unaiondeshea Marekani nafasi yake yakuwa “mdhamini na msuluhishi” wa mchakato wa amani Mashariki ya Kati.

Azimio hilo pia limesema kuwa uamuzi wa Trump katika suala la Jerusalem “umerudisha nyuma juhudi za kuleta amani, unaongeza mvutano na utazusha ghadhabu ambayo inahatarisha kuitumbukiza eneo hilo katika dimbwi la machafuko, vurugu na umwagaji damu.”

Mkuu wa Umoja wa nchi za Kiarabu ametaka mataifa yote duniani kuitambua Palestina kuwa taifa huru lenye makao makuu yake Jerusalem, kujibu tangazo alilolitoa Trump.

Mawaziri pia wametaka Baraza la Umoja wa Mataifa kupitisha azimio la kulaani uamuzi wa Trump.

Mkutano huo nchini Cairo umefanyika baada ya siku tatu za maandamano Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Ukanda wa Gaza

Wakati huo huo Shirika la habari la Uingereza BBC limeripoti kuwa Mataifa ya Kiarabu kwa pamoja yameitaka Marekani kubatilisha uamuzi wake wa kuitambua Jerusalem.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Lebanon, Gebran Bassil, alisema kuwa mataifa ya kiarabu, yanafaa kufikiria hatua ya kuiwekea Marekani vikwazo vya kiuchumi.

Amesema vikwazo hivyo vitasaidia kuzuia hatua hiyo ya kuhamisha makao makuu ya Israeli huko Jerusalem.

Bassil, amesema kuwa, hatua za kidiplomasia na kisiasa, zinafaa kuchukuliwa, kisha kufuatiwa na vikwazo vya kiuchumi na kifedha.

.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG