Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 04:25

Marekani yaiondoa Nigeria katika orodha ya wakiukaji wa kidini


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Nairobi, Kenya, Nov. 18, 2021, akielekea Abuja, Nigeria. (AP Photo/Andrew Harnik, Pool)
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Nairobi, Kenya, Nov. 18, 2021, akielekea Abuja, Nigeria. (AP Photo/Andrew Harnik, Pool)

Marekani imeiondoa Nigeria katika orodha ya wakiukaji wa kidini kabla ya ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken nchini humo.

Mwaka 2020 Marekani iliiweka Nigeria katika orodha ya uangalizi maalumu wa nchi ambazo zinakiuka au kupuuzia uhuru wa dini.

Nigeria haikuwa katika orodha ya mwaka 2021 iliyo na nchi za Myanmar, China, Eritrea, Iran, Korea Kaskazini, Pakistan, Russia, Saudi Arabia, Tajikistan na Turk-Menistan. Algeria, Comoro, Cuba na Nicaragua ambazo pia zipo katika orodha hiyo maalumu ya serikali ya Marekani ya nchi zinazokiuka uhuru wa dini, hiyo ni kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.

Hata hivyo kundi la kigaidi la Boko Haram na ISWAP yanayofanya operesheni kaskazini mwa Nigeria bado yapo katika uangalizi wa ukiukwaji huo.

Blinken anatembelea Nigeria leo katika siku ya pili ya ziara yake kwenye mataifa matatu ya Afrika ikiwemo Kenya na Senegal.

Anatarajiwa kukutana na Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari kujadiliana jinsi gani nchi hizo mbili zinaweza kushirikiana zaidi katika masuala ya afya ya dunia, usalama, nishati na ukuwaji wa kiuchumi.

XS
SM
MD
LG