Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 10, 2022 Local time: 04:47

Wajenzi wahofiwa kufa baada ya nyumba kuporomaka Lagos


Picha ya maktaba ya jengo lililoporomoka

Nchini Nigeria inaripotiwa kuwa takriban watu 100 Jumatatu wamekwama baada ya jengo la kifahari lililokuwa likijengwa kwenye eneo la makazi katika mji mkuu wa kibiashara wa  Lagos kuporomoka.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, wengi wa waliokwama kwenye vifusi vya jengo hilo ni wajenzi. Kufikia Jumatatu jioni mwili mmoja ulipatikana wakati manusura watatu waliokolewa, huku timu za uokozi zikiendelea na shughuli za uokozi.

Matukio ya majengo kuanguka ni suala la kawaida nchini Nigeria ambako sheria za ujenzi hazijingatiwi inavyohitajika. Mamlaka za mji wa Lagos zimesema kwamba jengo hilo lilikuwa na gorofa 22, na kwamba wanaendelea na ukaguzi wa majengo yalioko karibu ili kutadhmini iwapo yaliathiriwa. Jengo hilo linasemekana kuwa sehemu ya majengo mengine matatu yaliokuwa yakijengwa na kampuni ya Fourscore Homes.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG