Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Agosti 17, 2022 Local time: 10:55

Mumiliki wa jengo lililoporomoka Nigeria naye alifariki katika ajali hiyo


Wafanyakazi katika sehemu ya jengo lililoanguka Lagos, Nigeria.

Waokoaji wanaotafuta manusura katika jengo lililoanguka wakati wa ujenzi mjini Lagos Nigeria, wamepata mwili wa mwenye jengo hilo ndani ya mabaki ya jengo.

Watu wametambua mwili huo kuwa Olufemi Osibona, Tajiri aliyemiliki nyumba hiyo ya gorofa 21 iliyoanguka jumatatu.

Idadi kamili ya watu waliokufa katika mkasa huo haijajulikana.

Kufikia sasa, watu 36 wamethibitishwa kufariki.

Walioshuhudia tukio hilo wamesema kwamba watu 50 walikuwa katika jengo hilo wakati lilianguka.

Watu tisa pekee wameokolewa wakiwa hai. Maafisa wanachunguza kilichopelekea jengo kuanguka.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG