Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 09:45

Rais Buhari aruhusu utumiaji wa Twitter


Rais Muhammadu Buhari
Rais Muhammadu Buhari

Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria ameamuru kuondolewa marufuku ya utumiaji wa ukurasa wa mtandao wa Twitter nchini mwake lakini ikiwa tu kampuni hiyo kuu ya teknohama inatekeleza masharti fulani. 

Marufuku hiyo ilikuwa inaendelea kutekelezwa Ijumaa ingawa Rais Buhari amesema Wanigeria wanaweza kuanza kutumia jukwaa hilo kwa ajili ya biashara na mawasiliano chanya.

Katika hotuba ya kuadhimisha siku ya uhuru wa Nigeria kiongozi huyo alisema kwamba kamati ya ofisi ya rais imeanza kuwasiliana na wakuu wa Twitter juu ya masuala kadhaa kuanzia usalama wa kitaifa na ulipaji kodi unaostahiki na namna ya kutanzua ugomvi. Twitter haijajibu bado kuhusu matamshi ya rais.

Serikali ya Nigeria ilisitisha shughuli za Twitter mwezi Juni baada ya kampuni hiyo ya mitandao ya kijamii kufuta ujumbe wa rais Buhari.

Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali vya habari

XS
SM
MD
LG