Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 05, 2024 Local time: 02:18

Mauaji Nigeria : Buhari atoa wito kwa taifa kuungana


Rais Muhammadu Buhari
Rais Muhammadu Buhari

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ametoa wito kwa jamii kuungana ili kupunguza uhasama baada ya ghasia katika mji wa kati kuua dazeni za watu.

Jos, katika Jimbo la Plateau, katika miaka ya nyuma lilikumbwa na mapigano kati ya jamii za Waislamu na Wakristo.

Hata hivyo maafisa wa eneo hilo wanasema mashambulizi ya hivi karibuni ni kazi ya wahalifu badala ya vurugu za kidini.

Wasafiri wa Kiislam wasiopungua 23 waliuwawa mwanzoni mwa mwezi huu wakati msafara wao wa basi uliposhambuliwa nje ya Jos.

Polisi walisema watuhumiwa walikuwa ni kundi la wanamgambo wa Kikristo.

Zaidi ya wiki moja baadaye, watu wenye silaha walivamia kwenye kijiji kimoja kilicho na Wakristo wengi nje kidogo ya jiji, wakiwauwa watu 18 na kuchoma moto nyumba kadhaa.

XS
SM
MD
LG