Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 02:20

Cameroon yasema mamia ya wanamgambo wa Boko Haram wajisalimisha


Wanajeshi wa Cameroon wakishika doria kaskazini mwa nchi karubu na kijiji cha Mabass

Maafisa wa Cameroon Jumanne wamesema kuwa takriban wapiganaji wa zamani wa Boko Haram kutoka Nigeria na Chad, pamoja na familia zao, wamejisalimisha kwa mamlaka wiki iliyopita. Maafisa wanasema mamia ya waliojisalimisha karibuni miongoni mwao ni wanamgambo wa kiislamu. 

Cameroon Jumanne imesema kwamba kituo chake cha Kimataifa cha Usalimishaji Silaha, Uhamasishaji na Kuungana tena huko Meri, mji wa kasakzini kwenye mpaka na Nigeria, kuna wanamgambo wanajihadi 967 waliyojisalimisha. Wiki moja iliyopita, kulikuwa na kiasi cha wapiganaji wazamani 700 wa Boko Haram na familia zao katika kituo hicho.

Zaidi ya 260 waliowasili katika muda wa wiki moja iliyopita walikuwa wapiganaji 82 wa kiume wa zamani wa Boko Haram wakati wengine wakiwa ni wanawake na watoto.

Francis Fai Yengo ambaye ni mkurugenzi wa vituo vya DDR ambavyo vimeundwa na serikali ya Cameroon kwa ajili ya wapiganaji wa zamani, amesema zaidi ya 200 ni wanamgambo wa zamani wa Nigeria. Amesema baada ya kuzungumza na Rais Paul Biya, alimuomba kukutana na wanamgambo wa zamani na kutathmini mahitaji yao.

Yengo amesema kuwa wanamgambo kadhaa wa zamani ni raia wa Chad, akiongeza kuwa Biya ametoa fursa na ufadhili mkubwa zaidi kwa DDR kujengwa huko Meme, mji mwingine wa kaskazini usiyo mbali na Nigeria.

Yengo amesema kituo cha Meri kilikuwa kidogo mno kudhibiti ongezeko kubwa la idadi ya watu wanaowakimbia wanamgambo wa Boko Haram.

Kikosi cha pamoja kwenye bonge la Ziwa Chad kinachopambana na kundi la wanajihadi kimesema wanamgambo wa zamani wamejisalimisha wenyewe kwa wanajeshi kuzunguka msitu wa Sambisa kwenye mpaka wa Cameroon na Nigeria, eneo ambalo linasakidiwa ni ngome ya Boko Haram. Kikosi kazi hicho kinaundwa na wanajeshi kutoka Niger, Cameroon, Chad, na Nigeria.

Nigeria haijatoa taarifa za kueleza iwapo kuna wanamgambo wanaondoka kutoka kundi hilo. Cameroon inasema imewakabidhi kwa hiari wapiganaji wa zamani wa Nigeria mara kadhaa lakini idadi ya wale waliojisalimisha wiki hii ni kubwa zaidi.

Mapema mwezi huu,Cameroon imesema kwamba tangu May, pale kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau alipotangazwa amekufa, kundi hilo la wanajihadi na wapiganaji wake wamekuwa dhaifu na hivyo kuamua kujisalimisha.

Magaidi wa Boko Haram wamekuwa katika mapigano kutaka kusimika ukhalifa wa kiislamu kaskazini mashariki mwa Nigeria. Wapiganaji walianzisha mashambulizi ndani ya Cameroon mwaka 2014.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, watu 30,000 wameuawa na milioni 1.8 wamekoseshwa makazi nchini Cameroon, Nigeria na Chad tangu mwaka 2009 wakati mapigano yalipobadilika na kuwa mzozo wa silaha na wanajeshi wa serikali ya Nigeria.

XS
SM
MD
LG