Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 29, 2022 Local time: 05:12

Wanafunzi 15 Nigeria waliokuwa wametekwa waungana na familia zao


Mwanafunzi aliyekuwa ameweka na kuachiwa huru akiungana na familia yake katika Shule ya Sekondari ya Juu ya Bethel Baptist huko Damishi, Nigeria, Jumapili, Julai 25, 2021. (AP Photo).

Wanafunzi 15 wameungana tena na familia zao wiki saba baada ya kutekwa nyara kutoka shule yao kaskazini magharibi mwa Nigeria.

Mzazi mmoja anasema baadhi ya wanafunzi hao wako hospitali kwa matibabu baada ya kukumbwa na madhila hayo.

Kwa ujumla wanafunzi 121 walitekwa nyara kutoka shule ya sekondari ya Bethel Baptist katika jimbo la Kaduna na polisi wanasema juhudi zinaendelea kuwatafuta wanafunzi 65 ambao bado wanashikiliwa.

Kiongozi mmoja wa mji anasema fidia imetolewa ili kuachiliwa kwa wanafunzi lakini watekaji nyara wamewaachilia wachache kuliko idadi walioahidi.

Maafisa wa usalama wa Nigeria wameshiundwa kuzuia utekaji wa halaiki unaonedelea nchini humo zaidi ya wanafunzi elfu moja wameshatekwa tangu disemba.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG