Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 11, 2024 Local time: 00:12

Wanafunzi watekwa nyara Nigeria


Darasa lililobaki tupu baada ya wanafunzi kutekwa nyara kaskazini mwa Nigeria
Darasa lililobaki tupu baada ya wanafunzi kutekwa nyara kaskazini mwa Nigeria

Kiasi cha wanafunzi 150 hawajulikani walipo baada ya watu waliokuwa na silaha kuvamia shule ya bweni katika jimbo la kaduna nchini Nigeria.

Mzazi mmoja na afisa utawala wamesema Jumatatu kuwa polisi pamoja na wanajeshi wanawasaka, wanafunzi hao. Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, shule hiyo ya upili ya Bethel Baptist ni ya 10 kushambuliwa kaskazini magharibi mwa Nigeria tangu Decemba, wakati mamlaka zikisema kuwa washambuliaji hudai fidia baada ya kuwateka nyara wanafunzi.

Ripoti zinasema kuwa darzeni ya wazazi waliokuwa wakilia walikusanyika kwenye shule hiyo, wakitarajia kupata taarifa kuhusiana na waliko watoto wao. Ripoti za polisi zinasema kuwa washambuliaji waliingia saa za usiku na kuwashinda nguvu walinzi waliokuwepo huku wakitoroka na wanafunzi kuelekea kwenye msitu ulio karibu.

Hata hivyo taarifa zimeongeza kusema kuwa watu 26 akiwemo mwalimu mmoja wa kike wameokolewa. Mwanazilishi wa shule hiyo kasisi John Hayab ameiambia Reuters kwamba takriban watu 25 walibahatika kuponyoka wakati wanafunzi waliobaki walishikwa mateka na washambuliaji.

XS
SM
MD
LG