Maafisa wa usalama wa Nigeria wameokoa watu sita ambao walikuwa wametekwa nyara kutoka chuo kikuu karibu na uwanja mkuu wa ndege wa kimataifa.
Watu hao walitekwa nyara wakiwa katika chuo kikuu cha Abuja na kusababisha wasiwasi kuhusu hali ya usalama katika uwanja wa ndege wa Nnamdi Azikiwe, ulio kilomita 20 kutoka chuo hicho.
Msemaji wa polisi mjini Abuja Josephine Adeh, amesema kwamba watu waliokuwa wametekwa nyara wameokolewa.
Adeh amesema kwamba watu sita walitekwa nyara.
Chuo kikuu kimesema kwamba waliokuwa wametekwa nyara ni wafanyakazi wanne na Watoto wao.
Nigeria, yenye idadi kubwa ya watu Afrika, kiasi cha milioni 210, inakabiliwa na ukosefu wa usalama.
Makundi ya watu wenye silaha yameongeza mashambulizi dhidi ya shule na vyuo vikuu katika miezi ya hivikaribuni.
Kulingana na umoja wa mataifa, wanafunzi 950 wametekwa nyara na makundi ya watu wenye silaha tangu mwezi Desemba.