Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 07, 2023 Local time: 15:33

Wafungwa 446 wamekamatwa tena baada ya kutoroka gerezani huko Nigeria


Mfano wa jengo la magereza huko Nigeria
Mfano wa jengo la magereza huko Nigeria

Watu wenye silaha waliotumia mabomu walivamia gereza la Abolongo huko kusini magharibi mwa jimbo la Oyo mwishoni mwa Ijumaa kituo hicho kilisema katika mlipuko wa tatu kwenye gereza kubwa kwa mwaka huu katika taifa hilo lenye idadi kubwa ya watu barani Afrika

Vikosi vya usalama nchini Nigeria viliwakamata tena wafungwa 446 ambao walitoroka gerezani wakati wafungwa wengi walipotoroka gerezani mwishoni mwa juma na wengine karibu 400 bado wanatafutwa kufikia leo Jumatatu, maafisa walisema.

Wanaume wenye silaha kali waliotumia mabomu walivamia gereza la Abolongo huko kusini magharibi mwa jimbo la Oyo mwishoni mwa Ijumaa kituo hicho kilisema katika mlipuko wa tatu kwenye gereza kubwa mwaka huu katika taifa hilo lenye idadi kubwa ya watu barani Afrika.

Waziri wa mambo ya ndani wa Nigeria, Rauf Aregbesola, alisema wafungwa 446 wamekamatwa tena na 392 bado wanatafutwa baada ya kulitembelea gereza hilo Jumapili. Shambulizi hilo halikuweza kufahamika alisema.

Serikali kuu itawafuatilia sio tu wale walioshambulia kituo chetu, lakini pia wale waliokimbia kutoka gerezani, aliongeza. Unaweza kukimbia, lakini huwezi kujificha, waziri huyo alisema, akiongeza kwamba mipango ilikuwa ikiendelea kutoa maelezo ya kina juu ya wafungwa kupitia vyombo vya habari.

XS
SM
MD
LG