Kila mwaka, familia nchini Marekani zinawaleta majumbani maelfu ya watoto wanaotoka ndani na nje ya nchi kuwalea. Kumleta nyumbani mtoto mgeni inahitaji kumjengea mazoea. Kumleta nyumbani mtoto wa rangi tofauti inaleta changamoto nyingine katika malezi hayo.
Waandishi wa habari wa VOA kote ulimwenguni waliangaza maudhui yanayohusu thamani ya mtoto wa kike kuonyesha jinsi gani biharusi mtoto anavyothaminiwa na familia zote mbili : Ile anayoihama na nyingine anapoolewa. Na ni thamani gani anayolipa mtoto huyo wa kike anapoolewa akiwa chini ya miaka 18?
Kuna zaidi ya watu milioni 68.5 waliolazimishwa kukimbia makazi yao ulimwenguni na zaidi ya milioni 25 kati yao ni wakimbizi, kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi (UNHCR).
Michuano ya 31 ya mataifa ya Afrika ya mwaka 2017 inafanyika nchini Gabon. Michuano hii ni ya soka kwa wanaume ikiwa inaandaliwa na shirikisho la soka barani Afrika (CAF).
Mamilioni ya watu barani Afrika hawana uwezo wa kupata chakula cha kutosha. Somalia iko ukingoni mwa janga la njaa. Ukame nchini Kenya umesababisha serikali kutangaza hali ya hatari.
Kuhusu Mradi Huu Waandishi wa Idhaa ya Kiswahili VOA wameandaa Makala Maalum juu ya Uchaguzi Mkuu Kenya baada ya kuzungumza na wananchi katika ngazi mbalimbali wakati kampeni zinaendelea nchini humo.
Ajali za barabarani Afrika Mashariki zimekuwa moja ya majanga yanayogusa nchi hizo kwa kiwango kikubwa. Mwaka hadi mwaka idadi inaongezeka ya raia wanaopoteza maisha na wengine kupata ulemavu wa kudumu kutokana na ajali za njia za usafiri.
Wananchi wa Uganda watashiriki katika zoezi la kumchagua rais, wabunge na madiwani katika upigaji kura utakaofanyika Alhamisi 18 Ferbuari, 2016.
Mpango wa viongozi vijana uliobuniwa na Rais Obama (YALI) unawawezesha vijana kupitia elimu, mafunzo kwa vitendo, mafunzo ya uongozi na kubadilishana mawazo.
Ukurasa huu maalum unafuatilia ziara ya kwanza ya Rais Barack Obama wa Marekani nchini Kenya, nchi aliyotokea baba yake.