Duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais asiyekuwa na mamlaka makubwa, ilionekana kama mtihami kwa uchaguzi wa wabunge.
Gordana Siljanovska-Davkova, anayeungwa mkono wana vyama vya upinzani, alionekana kuwa msitari wa mbele katika uchaguzi huo.
Anakabiliana na rais wa sasa Stevo Pendarovski, anayeungwa mkono na muungano wa vyama vilivyo madarakani, vya mrengo wa kushoto.
Siljanovska-Davkova alipata asilimia 41, katika raundi ya kwanza iliyofanyika April 24, ikilinganishwa na asilimia 20.5 ya kura alizopata Pendarovski.
Wawili hao walikabiliana katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2019 ambapo Pendarovski alipata ushindi wa asilimia 54.
Ni lazimia asilimia 40 ya wapiga kura washiriki duru ya pili ndipo matokeo yakubalike.
Forum