Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 13, 2024 Local time: 22:38

Marekani imesitisha msaada wa mabomu kwa Israel


Rais wa Marekani Joe Biden akiwa katika mazungmzo na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu Oktoba 18, 2023
Rais wa Marekani Joe Biden akiwa katika mazungmzo na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu Oktoba 18, 2023

Marekani imesitisha upelekaji wa msaada wa mabomu kwa Israel kutokana na waiwasi kwamba Israel ilikuwa inakaribia kuushambulia mji wa Rafah, kusini mwa Gaza kinyume na matamanio ya Marekani.

Miongoni mwa sialha hizo ni mabomu yenye uzito wa kilogram 900, na kilogram 225.

Shirika la habari la AP limenukuu chanzo cha habari ambacho hakijatajwa kutokana na usiri wa habari hiyo.

Zaidi ya watu milioni 1 wanaishi katika mji wa Rafah baada ya kukimbia Gaza kutokana na mashambulizi ya Israel dhidi ya Hamas yaliyoanza baada ya wanamgambo wa Hamas kuishambulia Israel Oktoba 7.

Utawala wa rais wa Marekani Joe Biden, ulianza kuthathmini msaada wake wa silaha kwa serikali ya Benjamin Netanyahu, baada ya kuonekana kutaka kuivamia Rafah licha ya pingamizi kutoka White house.

Shinkizo dhidi ya Israel linaendelea kuongezeka

Qatar na umoja wa Afrika wameelezea wasiwasi kuhusu mgogoro wa kibinadamu unaoendelea katika mji wa Rafah, kusini mwa Gaza kutokana na Operesheni ya jeshi la Israel katika sehemu hiyo

Qatar imekuwa moja ya nchi zinazoongoza juhudi za upatanishi kutafuta makubaliano kati ya Israel na Hamas, naleo Jumatano imesema kulazimishwa kwa nguvu kuwakosesha makazi raia kutoka Rafah itakuwa ni ukiukaji mkubwa sana wa sheria za kimataifa.

Taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Qatar imelaani mashambulizi ya Israel huko Rafah na kutaka hatua za haraka za kimataifa kuchukuliwa kuwazuia wanajeshi wa Israel kuingia mjini humo.

Mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat, ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kufanya kazi pamoja na kuzuia vita katika mji wa Rafah akisema kwamba sehemu hiyo ni muhimu katika usafirishaji wa misaada ya kibinadamu kuingia Gaza.

Viongozi wa Israel wamesema kwamba operesheni ya kijeshi katika Rafah ni muhimu katika kufanikiwa kuwapata watu wanaoshikiliwa mateka na Hamas na kushinda nguvu kundi hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG