Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 02, 2024 Local time: 23:34

Idara ya kupambana na ufisadi ya Nigeria yapata zaidi ya dola milioni 25 zilizoibwa


Rais wa Nigeria, Bola Tinubu
Rais wa Nigeria, Bola Tinubu

Idara ya kupambana na ufisadi nchini Nigeria imesema kuwa tayari imepata karibu dola milioni 27 kufuatia uchunguzi dhidi ya waziri wa serikali aliyesimamishwa kazi, pamoja na maafisa wengine.

Rais Bola Tinubu alimsimamisha kazi waziri wa Masuala ya Kibinadamu na Kuangamiza Umasikini, Betta Edu, Januari mwaka huu, kufuatia tuhuma kwamba alielekeza fedha za umma kwenye akaunti binafsi za benki. Tinubu pia alimsimamisha kazi kiongozi wa uwekezaji wa jamii kwenye wizara hiyo Halima Shehu, kutokana na tuhuma za ufisadi.

Kwa mijibu wa shirika la habari la Reuters, Shehu alikamatwa na kisha kuachiliwa kwa dhamana. Taarifa zaidi zinasema kuwa aliyekuwa waziri wa wizara ya kupambana na umaskini Sadiya Umar Farouq, pia alikamatwa ili kusaidia kwenye uchunguzi. Tinubu tangu kuchukua madaraka mwaka uliopita amefanya marekebisho kadhaa ya kiuchumi, wakati pia akiwasimamisha kazi maafisa kadhaa serikalini, akiwemo gavana wa benki kuu Godwin Emefiele.

Forum

XS
SM
MD
LG