Hali imeendelea kuwa mbaya kwenye kisiwa hicho kutokana na idadi kubwa ya wahamiaji wanaowasili, huku maafisa wakiwahamisha wahamiaji wengine kuelekea Sicily.
Wahamiaji wanaendelea kuwasili Sicily, walitokea bandari za Mahdia, Sidimansour na Zazis nchini Tunisia.
Wengine wanatokea bandari za Zouara, Zawia, Zuwara, Zebrata, Saborata na Zaira nchini Libya.
Jumamosi, wahamiaji 438, wakiwemo Watoto 117 na wanawake 35, waliwasili kwenye bandari ya Taranto, kusini mwa Italia baada ya kuokolewa na meli ya uokoaji ya Ujerumani.
Facebook Forum