Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 05, 2024 Local time: 10:58

Wahamiaji 8 wafariki katika mwambao wa Morocco


Kijana muhamiaji, akiogelea karibu na uzio kati ya mpaka wa Uhispania na Morocco, Mei 19, 2021. Picha ya Reuters
Kijana muhamiaji, akiogelea karibu na uzio kati ya mpaka wa Uhispania na Morocco, Mei 19, 2021. Picha ya Reuters

Maafisa wa Morocco Jumatatu wameopoa miili ya wahamiaji wanane katika mwambao wa kusini mwa taifa hilo la kifalme la Afrika kaskazini, maafisa wa eneo hilo wamesema.

Boti yao ya kujazwa na hewa ilizama karibu na mji wa pwani wa Akhfennir katika mkoa wa Tarfaya ilipokuwa inajaribu kufika visiwa vya Canary nchini Uhispania, maafisa hao wamesema.

Wahamiaji wengine 18, wengi wao Waafrika, walinusurika na kuzuiliwa kwa mahojiano, maafisa hao wameongeza.

Morocco ni kitovu muhimu cha kusafiria kwenye njia zinazotumiwa na wahamiaji wanaotafuta maisha bora barani Ulaya.

Mwezi uliopita, watu 23 walifariki wakijaribu kupanda uzio wa mpaka kwenye eneo la Uhispania la Mellila, kwenye pwani ya Mediterania ya Morocco.

Shirika linalosaidia wahamiaji Caminando Fronteras linasema wahamiaji 1,000 walifariki au waliripotiwa kutoweka baharini katika nusu ya kwanza ya mwaka walipokuwa wakijaribu kufika Uhispania.

XS
SM
MD
LG