Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 11, 2024 Local time: 02:14

Wahamiaji waliojaribu kuingia Uhispania wapewa kifungo cha miaka 11 Morocco


Wahamiaji kutoka Morocco wakiwa kwenye kambi ya muda ya Uhispania ya Melilla.
Wahamiaji kutoka Morocco wakiwa kwenye kambi ya muda ya Uhispania ya Melilla.

Zaidi ya wahamiaji 30 Jumanne wamehukumiwa nchini Morocco kutokana na kujaribu kuruka uzio wa mpakani na eneo la Uhispania la Melilla mwezi Juni.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP. Hukumu hiyo ya miezi 11 jela kwa kila mmoja wao, imetolewa katika mahakama ya mji wa Nador, hatua iliyozua ukosoaji mkubwa kutoka kwa makundi ya kutetea haki za binadamu. Mamia ya wahamiaji walijaribu kuvuka kutoka Morocco wakielekea Melilla Juni 24, ambapo 23 kati yao walikufa kutokana na kile seriali ilitaja kuwa mkanyagano .

Kando na hukumu, wahamiaji hayo pia wameamrishwa kulipa faini ya dola 49 kila mmoja, pamoja na nyingine ya dola 340 za kugharamia mashitaka kutoka kwa maafisa wa huduma za umma waliowasilisha kesi dhidi yao. Mashirika yasio ya kiserikali yamelalamikia hatua hiyo huku shirika la Morocco la kutetea haki za binadamu la AMDH likiomba mahakama ya rufaa kubatilisha uamuzi huo. Mwezi Juni jumla ya wahamiaji 133 walikiuka amri za mpakani kati ya Morocco na Spain, ukiwa uvukaji wa kwanza wa halaiki tangu mataifa hayo kurejesha uhusiano wa kidiplomasia mwezi Mei.

XS
SM
MD
LG